Mhu. 3:20-22 Swahili Union Version (SUV)

20. Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

21. Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?

22. Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.

Mhu. 3