28. akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.
29. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.
30. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?
31. Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.