1. Hata Festo alipokwisha kuingia katika uliwali, baada ya siku tatu akapanda kwenda Yerusalemu kutoka Kaisaria.
2. Kuhani Mkuu na wakuu wa Wayahudi wakampasha habari za Paulo, wakamsihi,
3. na kumwomba fadhili juu yake, kwamba atoe amri aletwe Yerusalemu, wapate kumwotea na kumwua njiani.