Mdo 21:21-24 Swahili Union Version (SUV)

21. Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi.

22. Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja.

23. Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri.

24. Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.

Mdo 21