17. Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
18. Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.
19. Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;
20. bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
21. Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.