Mdo 14:23-25 Swahili Union Version (SUV)

23. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.

24. Wakapita kati ya Pisidia wakaingia Pamfilia.

25. Na baada ya kuhubiri lile neno katika Perge wakatelemka mpaka Atalia.

Mdo 14