Lk. 7:47-50 Swahili Union Version (SUV)

47. Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.

48. Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.

49. Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi?

50. Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani.

Lk. 7