17. BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako.
18. Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako.
19. Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
20. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.
21. BWANA akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba;