1. Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2. na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.