Kum. 26:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa BWANA, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi BWANA aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa.

4. Naye kuhani atakipokea kikapu mkononi mwako, akiweke chini mbele ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako.

5. Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.

6. Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito.

7. Tukamlilia BWANA, Mungu wa baba zetu; BWANA akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu.

8. BWANA akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu;

Kum. 26