7. Jinsi ilivyo mizuri juu ya milimaMiguu yake aletaye habari njema,Yeye aitangazaye amani,Aletaye habari njema ya mambo mema,Yeye autangazaye wokovu,Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
8. Sauti ya walinzi wako!Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja;Maana wataona jicho kwa jicho,Jinsi BWANA arejeavyo Sayuni.
9. Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja,Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa;Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,Ameukomboa Yerusalemu.
10. BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifuMachoni pa mataifa yote;Na ncha zote za duniaZitauona wokovu wa Mungu wetu.
11. Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.