2. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
3. Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye,Itengenezeni nyikani njia ya BWANA;Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
4. Kila bonde litainuliwa,Na kila mlima na kilima kitashushwa;Palipopotoka patakuwa pamenyoka,Na palipoparuza patasawazishwa;
5. Na utukufu wa BWANA utafunuliwa,Na wote wenye mwili watauona pamoja;Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.