Isa. 38:15-20 Swahili Union Version (SUV)

15. Niseme nini? Yeye amenena nami,na yeye mwenyewe ametenda hayo;Nitakwenda polepole miaka yangu yote,kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.

16. Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi;Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote;Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.

17. Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu;Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu;Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

18. Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu;mauti haiwezi kukuadhimisha;Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.

19. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo;Baba atawajulisha watoto kweli yako.

20. BWANA yu tayari kunipa wokovu.Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu,Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.

Isa. 38