Isa. 12:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Na katika siku hiyo utasema,Ee BWANA, nitakushukuru wewe;Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,Hasira yako imegeukia mbali,Nawe unanifariji moyo.

2. Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;Nitatumaini wala sitaogopa;Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;Naye amekuwa wokovu wangu.

3. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.

Isa. 12