Hos. 4:15-19 Swahili Union Version (SUV)

15. Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-Aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo BWANA.

16. Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! BWANA atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye nafasi!

17. Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache.

18. Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu.

19. Upepo umemfunikiza kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao.

Hos. 4