Hes. 7:58-61 Swahili Union Version (SUV)

58. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

59. tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

60. Siku ya kenda Abidani mwana wa Gideoni, mkuu wa wana wa Benyamini;

61. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

Hes. 7