Hes. 7:44-49 Swahili Union Version (SUV)

44. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

45. na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

46. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

47. tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Eliasafu mwana wa Deueli.

48. Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efraimu;

49. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

Hes. 7