2. Fanyeni hesabu ya mkutano wote wa wana wa Israeli, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mtu mume kichwa kwa kichwa;
3. tangu mwenye miaka ishirini umri wake, na zaidi, wote wawezao kutoka kwenenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kuandama majeshi yao.
4. Tena mtu mume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha nyumba ya baba zake.
5. Na majina ya hao waume watakaosimama pamoja nanyi ni haya; Wa Reubeni; Elisuri mwana wa Shedeuri.
6. Wa Simeoni; Shelumieli mwana wa Suri-shadai.
7. Wa Yuda; Nashoni mwana wa Aminadabu.