15. Ndipo akaniambia, Tazama, nimekupa mashonde ya ng’ombe badala ya mashonde ya mwanadamu, nawe utakipika chakula chako juu ya hayo.
16. Tena akaniambia, Mwanadamu, tazama, nitalivunja tegemeo la chakula katika Yerusalemu; nao watakula mkate kwa kuupima, na kwa kuutunza sana; nao watakunywa maji kwa kuyapima, na kwa kushangaa;
17. wapate kupungukiwa na mkate na maji, na kustaajabiana, na kukonda kwa sababu ya uovu wao.