Eze. 35:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena neno la BWANA likanijia, kusema,

2. Mwanadamu, kaza uso wako juu ya mlima Seiri, ukatabiri juu yake,

3. uuambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima Seiri, nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, nami nitakufanya kuwa ukiwa na ajabu.

4. Miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Eze. 35