Eze. 19:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena uwaombolezee wakuu wa Israeli,

2. useme, Mama yako alikuwa nini? Simba mke; alijilaza kati ya simba, kati ya wana-simba aliwalisha watoto wake.

3. Akamlea mtoto mmoja katika watoto wake, akawa mwana-simba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu.

Eze. 19