Efe. 5:6-11 Swahili Union Version (SUV)

6. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.

7. Basi msishirikiane nao.

8. Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,

9. kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;

10. mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.

11. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;

Efe. 5