Ebr. 8:11-13 Swahili Union Version (SUV)

11. Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake,Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana;Kwa maana wote watanijua,Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12. Kwa sababu nitawasamehe maovu yao,Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

13. Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

Ebr. 8