7. Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
8. na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;
9. naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
10. kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.