Ayu. 6:20-24 Swahili Union Version (SUV)

20. Wametahayari kwa sababu walitumaini;Wakaja huku, nao walifadhaika.

21. Kwani sasa ninyi mmekuwa vivyo;Mwaona jambo la kutisha, mkaogopa.

22. Je! Nilisema, Nipeni?Au, Nitoleeni toleo katika mali yenu?

23. Au, Niokoeni na mkono wa adui?Au, Nikomboeni na mikono ya hao waoneao?

24. Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya;Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.

Ayu. 6