7. Wakati nilipotoka kwenda mjini, hata langoni,Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
8. Hao vijana waliniona wakajificha,Nao wazee wakaniondokea na kusimama;
9. Wakuu wakanyamaa wasinene,Na kuweka mikono yao vinywani mwao;
10. Sauti yao masheki ilinyamaa,Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.
11. Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia;Na jicho liliponiona, likanishuhudia.
12. Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia;Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
13. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia;Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
14. Nalijivika haki, ikanifunika,Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.
15. Nalikuwa macho kwa kipofu,Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.