Ayu. 28:25-28 Swahili Union Version (SUV)

25. Apate kuufanyia upepo uzito wake;Naam, anayapima maji kwa kipimo.

26. Hapo alipoiwekea mvua amri,Na njia kwa umeme wa radi.

27. Ndipo alipoiona na kuitangaza;Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.

28. Kisha akamwambia mwanadamu,Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima,Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

Ayu. 28