19. Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho;Hufunua macho yake, naye hayuko.
20. Vitisho vyampata kama maji mengi;Dhoruba humwiba usiku.
21. Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka;Na kumkumba atoke mahali pake.
22. Kwani Mungu atamtupia asimhurumie;Angependa kuukimbia mkono wake.
23. Watu watampigia makofi,Na kumzomea atoke mahali pake.