Ayu. 26:9-12 Swahili Union Version (SUV)

9. Husitiri uso wa kiti chake cha enzi,Na kulitandaza wingu lake juu yake.

10. Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji,Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.

11. Nguzo za mbingu zatetemeka,Na kustaajabu kwa kukemea kwake.

12. Huichafua bahari kwa uwezo wake,Na kumtema Rahabu kwa akili zake.

Ayu. 26