Ayu. 23:14-17 Swahili Union Version (SUV)

14. Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa;Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.

15. Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake;Nitakapofikiri, namwogopa.

16. Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia,Naye Mwenyezi amenitaabisha;

17. Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza,Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.

Ayu. 23