Ayu. 12:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2. Hapana shaka ninyi ndinyi watu halisi,Nanyi mtakapokufa, ndipo na hekima itakoma.

3. Lakini mimi pia, nina fahamu kama ninyi;Mimi si duni yenu ninyi;Naam, ni nani asiyejua mambo kama hayo?

Ayu. 12