24. Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote;Mkewe Heberi, Mkeni,Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani.
25. Aliomba maji, naye akampa maziwa.Akamletea siagi katika sahani ya heshima.
26. Akanyosha mkono wake akashika kigingi,Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi;Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake.Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake.
27. Miguuni pake aliinama, akaanguka, akalala.Miguuni pake aliinama, akaanguka.Hapo alipoinama, ndipo alipoanguka amekufa.