Amu. 1:22-24 Swahili Union Version (SUV)

22. Nyumba ya Yusufu nayo, wao nao walikwea kwenda juu ya Betheli; naye BWANA alikuwa pamoja nao.

23. Kisha mbari ya Yusufu wakatuma watu waende kuupeleleza Betheli. (Jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Luzu.)

24. Hao wapelelezi walimwona mtu atoka katika huo mji, wakamwambia, Tafadhali, utuonyeshe maingilio ya mji huu, nasi tutakutendea mema.

Amu. 1