2 Sam. 16:16-20 Swahili Union Version (SUV)

16. Ikawa, Hushai, Mwarki, rafiki wa Daudi, alipomjia Absalomu, Hushai akamwambia Absalomu, Na aishi mfalme, aishi mfalme.

17. Naye Absalomu akamwambia Hushai, Je! Huu ndio wema wako kwa rafiki yako? Mbona hukutoka pamoja na rafiki yako?

18. Hushai akamwambia Absalomu, La, sivyo; lakini yule BWANA aliyemchagua, na watu hawa, na watu wote wa Israeli, mimi nitakuwa wake, na pamoja naye nitakaa.

19. Na tena, Ni nani ambaye yanipasa nimtumikie? Hainipasi kutumika mbele ya mwanawe? Kama nilivyotumika mbele ya baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mbele yako.

20. Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa shauri lako, tufanyeje.

2 Sam. 16