2 Sam. 1:15-21 Swahili Union Version (SUV)

15. Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa.

16. Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.

17. Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya;

18. (kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema,Wana wa Yuda na wafundishwe haya,

19. Walio fahari yako, Ee IsraeliJuu ya mahali pako palipoinuka wameuawa;Jinsi mashujaa walivyoanguka!

20. Msiyahubiri mambo haya katika Gathi,Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni;Wasije wakashangilia binti za Wafilisti,Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.

21. Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenuUmande wala mvua, wala mashamba ya matoleo;Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa,Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.

2 Sam. 1