2 Nya. 5:7-11 Swahili Union Version (SUV)

7. Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la BWANA mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.

8. Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu.

9. Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo.

10. Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.

11. Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao;

2 Nya. 5