2 Nya. 13:20-22 Swahili Union Version (SUV)

20. Wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha BWANA akampiga, akafa.

21. Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita.

22. Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

2 Nya. 13