2 Kor. 2:8-11 Swahili Union Version (SUV)

8. Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu.

9. Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote.

10. Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo,

11. Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

2 Kor. 2