6. Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.
7. Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.
8. Hezekia akamwambia Isaya, Je! Kutakuwa na ishara gani ya kwamba BWANA ataniponya, nami siku ya tatu nitapanda nyumbani kwa BWANA.