2 Fal. 12:11-14 Swahili Union Version (SUV)

11. Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya BWANA; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya BWANA,

12. na hao waashi, na wakata mawe, tena kununua miti na mawe ya kuchongwa, ili kuyatengeneza mabomoko ya nyumba ya BWANA, tena kwa gharama zote za kuitengeneza nyumba.

13. Lakini havikufanywa kwa nyumba ya BWANA vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyo vyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA;

14. kwa sababu hiyo fedha waliwapa watenda kazi, wakaitengeneza kwayo nyumba ya BWANA.

2 Fal. 12