1 Sam. 8:20-22 Swahili Union Version (SUV)

20. ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu.

21. Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA.

22. BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake.

1 Sam. 8