1 Sam. 8:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.

2. Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.

3. Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.

4. Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;

1 Sam. 8