1 Sam. 3:16-20 Swahili Union Version (SUV)

16. Basi Eli akamwita Samweli, akasema, Samweli, mwanangu. Naye akajibu, Mimi hapa.

17. Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Mungu akufanyie vivyo hivyo, na kuzidi, ukinificha lo lote katika hayo yote BWANA aliyosema nawe.

18. Basi Samweli akamwambia kila neno, asimfiche lo lote. Naye akasema, Ndiye BWANA; na afanye alionalo kuwa ni jema.

19. Samweli akakua, naye BWANA alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini.

20. Nao Waisraeli wote, toka Dani mpaka Beer-sheba, walitambua ya kwamba huyo Samweli amewekwa kuwa nabii wa BWANA.

1 Sam. 3