1 Pet. 3:8-13 Swahili Union Version (SUV)

8. Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;

9. watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

10. Kwa maana,Atakaye kupenda maisha,Na kuona siku njema,Auzuie ulimi wake usinene mabaya,Na midomo yake isiseme hila.

11. Na aache mabaya, atende mema;Atafute amani, aifuate sana.

12. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,Na masikio yake husikiliza maombi yao;Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.

13. Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?

1 Pet. 3