7. Na wa wana wa Benyamini; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;
8. na Ibneya, mwana wa Yerohamu; na Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu, mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya;
9. na ndugu zao, sawasawa na vizazi vyao; watu mia kenda na hamsini na sita. Watu hao wote ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, kwa kadiri ya mbari za baba zao.
10. Na katika makuhani; Yedaya, na Yehoyaribu, na Yakini;
11. na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;