18. wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;
19. wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeromothi mwana wa Azrieli;
20. wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila ya Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;
21. wa nusu kabila ya Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;
22. wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao walikuwa maakida wa kabila za Israeli.
23. Lakini Daudi hakufanya hesabu yao wenye miaka ishirini na waliopungua; kwa kuwa BWANA alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni.