14. Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.
15. Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.
16. Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.
17. Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
18. Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.
19. Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
20. Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21. Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.
22. Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.