1 Nya. 18:12-15 Swahili Union Version (SUV)

12. Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu.

13. Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda.

14. Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.

15. Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.

1 Nya. 18